FPCT ina makanisa ya mahali (Local Churches) 192, ina zaidi ya parishi 850 na matawi zaidi ya 4500 kote nchini. Haya yote yanaendelea kukua na baadaye kuwa makanisa ya mahali. FPCT ina idara nane zinazotoa huduma za kimwili, kiakili na kiroho kwa jamii ya watanzania.Hata hivyo makadirio ni kati ya 400,000 na kuendelea. Kanisa limejiwekea mpango mkakati wa uendeshaji kazi wa miaka 10 kuanzia 2014-2024, ambao utasambazwa katika makanisa yote, idara na taasisi kwa utekelezaji.MAONO (DIRA) YA FPCT (FPCT VISION STATEMENT)Maono ya FPCT ni kuwa na kanisa linalojiongoza,linalojitegemea na linalojieneza, likifanya kazi kwa umoja unaowakilisha umoja katika Kristo.TAMKO LA KIMISHENI (MISSION STATEMENT)Kuhubiri, kueneza Injili ya Kristo kwa maneno na matendo, kuwafanya wote watakaoamini kuwa wanafunzi wa Yesu, hivyo kutimiza agizo kuu la Bwana wetu Yesu Kristo.Kupata kurasa zingine, Bofya chini next page aligned left …
http://fpct.or.tz/orodha-ya-makanisa-fpct/#comment-67
No comments:
Post a Comment