Maelezo Yanajitoxheleza
Povu Ruksa Wapendwa
"Wala hata Simlaumu DIAMOND PLATNUMZ juu ya Wimbo wa HALELUYAH"
Povu Ruksa Wapendwa
"Wala hata Simlaumu DIAMOND PLATNUMZ juu ya Wimbo wa HALELUYAH"
Nimeshuhudia Post nyingi sana za Kumshutumu, kitu ambacho kinatakiwa ni kuelimishwa aweze kutambua, HALELUYAH maana yake ni nini, na Je! wanaopaswa kulitumia neno hili HALELUYAH ni kina nani na wapi? Usimlaumu mtu kabla hujamwambia ubaya wa Jambo ambalo amelifanya, YESU alisema
👇
Yohana 15:22 Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao.
Kitu cha msingi ni kusema nae, ajue ili asiwe na udhuru wa Dhambi yake, nimesema kuwa sitamlaumu bali nampongeza sana, kwa sababu amewafanya watu WENGI wajue kuwa, HALELUYA, haipaswi kufanyiwa Mizaha, kwa sababu, HALELUYA maana yake ni "MSIFUNI BWANA" maandiko yanasema
👇
Zaburi 149:1 Haleluya. Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.
DIAMOND anapaswa kuelimishwa kuwa, anatakiwa kumwimbia MUNGU, na siyo kutumia HALELUYA kwenye Kumsifu Demu wake, pengine ameona FILAMU kibao watu waovu pengine kuliko hata yeye, Wanaigiza UCHUNGAJI, na wanatumia Neno HALELUYA, Viongozi wa Makanisa wapo KIMYA, hawakemei, sasa Diamond akiona hivyo, na watu wenyewe kwenye Show zake wanaenda, anaona ni kawaida tu Neno HALELUYA kutumika, Japo maandiko yanasema
👇
Zaburi 150:1 Haleluya. Msifuni MUNGU katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.
2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6 Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA. Haleluya.
"KILA MWENYE PUMZI NA AMSIFU BWANA HALELUYAH" Diamond anayo pumzi, ana haki ya kumsifu BWANA, ila masharti yake ni haya
👇
ZABURI 33:1 Mpigieni BWANA vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
Kila Mwenye Pumzi aliye mnyofu wa moyo huyo ndiye anaepaswa kumsifu BWANA (HALELUYAH) Kuna uwezekano mkubwa DIAMOND hajui hivyo, ni jukumu la Wanaojua kumwelewesha, aelewe! asije kuchukulia kama Mazoea, kwa sababu Hata NENO MASHA 'ALLH hutumika katika nyimbo mbalimbali, masharti yana tofautiana, Kwenye HALELUYAH kunawapasa Wanyofu wa MOYO!
Siyo tu kwa DIAMOND, hata kwa waimbaji wa nyimbo za Injili, nao hawastahili kumsifu MUNGU, ikiwa hawana UNYOFU wa MOYO, maana tunaambiwa
👇
2 Timotheo 2:19 Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, BWANA awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la BWANA na auache uovu.
DIAMOND akitaka kumsifu BWANA (HALELUYA) anatakiwa auache UOVU! vivyo hivyo na kwa, WACHUNGAJI, MITUME NA MANABII, WAINJILISTI, WACHUNGAJI NA WAALIMU, mashemasi, Maaskofu, Mapdre, na Mastister, Maparoko, Makatekista, Wana choir, na Waimbaji Binfsi, Nk. Wanatakiwa wauache Uovu ili Wapate haki ya Kumsifu BWANA (HALELUYAH) tusikomae tu na DIAMOND, wakati hata Makanisa wapo kina DIAMOND wengi, kwanza tuwashughulikie waliopo kwetu, hao wa Nje, MUNGU atawashughulikia mwenyewe.
👇
1 Korintho 5:12 Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani?
13 Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu.

No comments:
Post a Comment